Muungano wa Kimataifa wa Mashirika ya Wagonjwa wa Magonjwa ya Ngozi (unaojulikana pia kama GlobalSkin) unashirikiana na watafiti katika Chuo Kikuu cha Cardiff (Uingereza) na Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Hamburg-Eppendorf (Ujerumani) kuhusu mradi wa Uchunguzi wa Kimataifa wa Athari ya Magonjwa ya Ngozi (GRIDD).
Utafiti wa GRIDD unalenga kukusanya data ya kimataifa kuhusu athari ya maradhi ya ngozi kwa maisha ya wagonjwa. Ni mradi wa kwanza wa uchunguzi wa athari wa kimataifa, ulioanzishwa na mgonjwa na unaoongozwa na mgonjwa kuhusu magonjwa ya ngozi na ambao unapima athari ya kweli ya magonjwa ya ngozi kutoka kwa mtazamo wa mgonjwa. Unaweza kupata habari zaidi kuhusu mradi huo hapa.
Kama mtu anayeishi na maradhi ya ngozi, tunakukaribisha na kukushukuru kwa nia yako ya kushiriki katika mradi huu wa kipekee wa uchunguzi ambapo wewe ndiye mtaalamu na maoni yako ni muhimu.
Utafiti utakuchukua takriban dakika 10 hadi 20 kukamilisha. Usiwe na wasiwasi ikiwa unahitaji muda zaidi - unaweza kuhifadhi majibu yako na uingie kwenye akaunti tena baadaye.
Ili kutimiza masharti yetu ya kimaadili, utahitaji kusoma Hati ya Taarifa kwa Mgonjwa na utoe idhini kabla ya kushiriki katika utafiti huu. Pia utahitaji kusajili akaunti katika jukwaa hili ili kufikia utafiti. Majibu yako katika utafiti hayatabainisha utambulisho kwani tutahifadhi herufi za kwanza za jina lako na barua pepe yako mbali na jibu lako.
Tafadhali bofya kiungo kilicho hapa chini ili kuanza. Utaelekezwa katika kila mojawapo ya hatua hizi na kwa utafiti.